AUDIO:Bashe Awataka Wabunge Kuacha Unafiki
Dodoma.Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amewataka wabunge kuacha unafiki kuhusu usalama kuwateka watu na kwamba yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa wakati wa mkutano Mkuu wa CCM.
Hivyo amesema kama wanataka wamfukuze CCM.
Bashe alikuja juu baada Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji yanafanywa na usalama wa Taifa.
Mwananchi