-->

Baraka Amtaja Mfalme wa Hip Hop Bongo

Msanii Baraka The Prince amefunguka na kusema rapa Lord Eyes kutoka Weusi ambaye pia ni msanii aliye chini ya usimamizi wake ndiye mfalme wa hip hop Bongo.

Baraka The Prince amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV na kusema wasanii ambao wana ‘diss’ yeye kumsimamia Lord Eyes katika kazi zake ni wale ambao wanaogopa ujio wa rapa huyo katika muziki na kusema watu hao wanajua uwezo wa Lord Eyes hivyo kinawatisha kuona sasa anarudi.

“Ukiondoa mimi kufanya biashara na Lord Eyes mimi ni shabiki wake namba moja, nimesikiliza ngoma zake nyingi sana unaona ni ngoma kali sana sema jamaa alikosa usimamizi tu wa kazi zake, nimesikia kuna watu wana ‘diss’ Lord Eyes kusimamiwa kazi zake na mimi nachoweza kusema hao ni waoga wanajua Lord Eyes ana talent kubwa hivyo wameanza kumuogopa, mimi namuona Lord Eyes ni mfalme wa hip hop Bongo” alisema Baraka The Prince

Baraka akiwa na Lord Eyez

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364