-->

Ben Pol Awaomba Radhi Mashabiki, Kisa Hiki Hapa

Msanii Ben Pol ambaye siku kadhaa zilizopita alikuwa mbogo kwa mtangazaji wa kipindi cha eNewz ya EATV, baada ya kuulizwa maswali kuhusu familia yake hususani mwanamke aliyezaa naye pamoja na mtoto, msanii huyo ameomba radhi kwa kitendo hicho.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Ben Pol amesema kuwa hakutegemea kufanya jambo hilo na kusema yeye kama binadamu kuna wakati anaweza kuamka vibaya asiwe na mood nzuri, hivyo anadai kuwa huenda angekuwa na team ingekuwa rahisi kumwongoza na kuepusha mambo kama hayo.

“Unajua siku hazifanani kuna siku nyingine unaweza kuamka uko down, kuna siku nyingine unaweza kuamka hauko poa sana ukashindwa kuzuia hisia zako, na muda mwingine unakuta haupo na team yako maana kama ungekuwa kwenye mazingira ya show huenda meneja angekuzia usifanye Interview utulie tu, lakini ndiyo hivyo umeamka umepata ugeni mtu amekuomba uongee naye ndiyo hayo yanatokea” alisema Ben Pol 

Ben Pol aliamua kutumia nafasi hii kuomba radhi kwa watu ambao walikwazika kuona kile kitendo kutoka kwake na kusema yeye kama binadamu pia hukosea muda mwingine

“Niseme nichukue nafasi hii kuomba ladhi kwa ambao wameitazama vibaya na kuona kama haikukaa vizuri, au kwa mtu ambaye imemkwaza au kama imeleta image yoyote mbaya nitumie pia nafasi hii kuomba ladhi, unajua kama binadamu kuna mahali tu utateleza lazima ukubali hilo hauwezi kuwa unapatia wewe kila siku, kuna siku unaweza kufanya maamuzi ambayo kesho yake unajiuliza kwanini nilifanya hiki” alisema Ben Pol 

Mtazame hapa jinsi alivyopaniku siku hiyo

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364