-->

Ben Pol Hataki Kuulizwa Kuhusu Ebitoke

Msanii wa RnB Bongo, Ben Pol ameweka wazi kuwa kwa sasa hapendi kuulizwa maswali kuhusu Ebitoke, mtoto na mahusiano.

Muimbaji huyo amesema kutokana na kazi zake ambazo anataka kuzifanya kwa sasa inamlazimu kufanya hivyo.

“Kwa series ya kazi zangu zinazokuja ningependa sana vitu binafsi nisiviongelee zaidi au hadi pale nitakapokuwa tayari kuzungumzia Ben Pol anafanya nini sasa hivi nianze kuzungumzia,” Ben Pol ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo sipo comfortable sana kusema vitu binafsi mahusiano, sijui mtoto nataka kupunguza kuvizungumzia hivyo vitu kwa sasa hivi kusema kweli,” amesisitiza.

Ben Pol ambaye anadai kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji Ebitoke amebainisha hilo ili kufanya uhusiano wao kuwa binafsi zaidi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364