-->

Bill Nass Afunguka Kinachoendelea Kati ya Wakazi na Godzilla

Bill Nass

Story kubwa ambayo inatrend kwenye Bongofleva ni kudaiwa kuwepo kwa vita ya maneno kati ya Wakazi na Godzilla ambapo kila mmoja kwa nyakati tofauti amejinadi kuwa ni bora zaidi ya mwingine kitu kilichopelekea kutoa nyimbo zinazosemwa wanaimbana.

Inadaiwa pia kutokana na vita hiyo ya maneno kumewafanya wasanii hao kutunga nyimbo za tambo mbapo wakati Wakazi akitoa wimbo aliouita Zillnass naye Godzilla ameachia wimbo unaoitwa Power.

Story ni kwamba eo June 19, 2017 kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongofleva anayedaiwa kumpa stress Godzilla na mkali wa hit song Mazoea, Bill Nass amefunguka akielezea namna alivyipokea issue hiyo.

>>>“Kwa muziki kama wa Hip Hop vitu kama diss track ni lazima tutegemee vinaweza kutokea muda wowote na kumuhusisha mtu yeyote. Kwa hiyo, kwangu mimi naona ni moja ya element za muziki wa Hip Hop kwani ku-diss ni kama mtu anafanya freestyle battle na mwingine anaweza kujibu pia.

“Bongo hazifanyiki sana diss track ila sisi wasanii tunasemana sana. Mtu akikaa pembeni anasema Bill Nass hana hiki. Sisi watu wa Hip Hop tunakuwa na msuguano wa hiyvo lakini kwa wenzetu ni changamoto ya kawaida sana kila mtu ana mtazamo wake.” – Bill Nass

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364