-->

Steve Nyerere Atoboa Siri ya Bongo Fleva Kuwafunga Bongo Movie

Jumapili hii timu ya mpira wa miguu ya wasanii wa Bongo Fleva ilitoana jasho na timu ya wasanii wa Bongo movie, lengo ikiwa ni kukusanya pesa za kuchangia waathirika wa maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

steve-nyerere

 

Katika mchezo huo, Bongo Fleva waliibuka washindi, wakiendeleza kipigo kwa Bongo Movie kwa mwaka wa 5 sasa mfululizo.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa sare ya 1-1, na kuingia katika mikwaju ya penati na Bongo Movie kupoteza penati moja iliyowanyima ushindi .

Akipiga story na eNewz Steve Nyerere akiwakilisha timu ya Bongo Movie aliwapaka matope Bongo Fleva kuwa wanashinda kwa uchawi, alisema “Tulivyofika hapa tulijiona kabisa fiziko za utumbo zimefeli hata sisi hatupendi kufungwa lakini wanaroga na sasa tumekubali kufungwa”.

Mechi hiyo ilisindikizwa na mechi ya timu ya wabunge washabiki wa Yanga wakikipiga na timu ya wabunge washabiki wa Simba katika uwanja wa Taifa, Wabunge wa Yanga wakishinda 5 – 2 dhidi ya Simba.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364