Chid Benz Afunguka Kuhusu Kurudia Tena Madawa
Rapa Chid Benz ambaye kipindi cha nyuma alikuwa akitumia madawa ya kulevya na baadaye alipelekwa rehabu kwa ajili ya kuacha matumizi ya madawa hayo amefunguka na kusema kuwa arudie kwenye matumizi ya madawa hayo au asirudie hilo watu wasiangalie.
Amesema yeye anatambua kuwa hawaangushi mashabiki zake kwenye ile kazi ya muziki ambayo ilifanya wamjue.
Chid Benz alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema kuwa mashabiki zake hawajali maneno ya mtaani yanayosemwa kuwa amerudia kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kusema maadui zake ndiyo watu ambao wanasambaza maneno hayo.
“Watu wananipenda kuliko kawaida, hata hayo maneno sijui nimerudia kwenye madawa ya kulevya yaani hata hawajali kabisa ila maadui zangu ndiyo wanajali maneno ila watu wangu hata nikitoka sina nguo wao wanaona mimi nimevaa nguo na watabisha hivyo yaani, hayo maneno wanayosema karudia nawaambia kuwa nirudie nisirudie, nifanye nisifanye sijali, mimi nafanya kazi ambayo wananchi walinijua kupitia kazi hii hivyo siwezi kuharibu hata kidogo, nitumie nisitumie sitakosea kufanya ile kitu wananchi walinijua nikifanya” alisema Chid Benz
eatv.tv