-->

Chura Ameniunganisha na Watu -Snura

Msanii wa muziki Bongo Snura Mushi a.k.a Snura amefurahishwa na mashabiki aliowapata wakati anatoa nyimbo ya chura mwaka jana mwezi wa nne.

Snura ameeleza kufurahishwa kwa kuongeza idadi ya mashabiki hao kupitia kipindi cha EIGHT cha TVE kuwa nyimbo yake ya chura ilimuwezesha kupata mashabiki wengi katika soko lake la muziki na anaimani bado anao mashabiki zake hao ambao wanaongezeka .

”Nilishitushwa sana na producer Don Jazzy alivyo post video anaimba nyimbo yangu ya chura, nakumbuka aliposti pia hata video yake kwenye Instagram yake,Pia meneja wake Lil Wayne alipost pia nyimbo ya chura nilifurahi kuona watu wameielewa” alisema Snura.

Nyimbo ya chura ilifungiwa na BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) mwezi wa tano, kutokana na kukosa maadili.

Na Laila Sued

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364