-->

Darasa Atoboa Sababu za Yeye Kufanya Vizuri

Rapa Darasa ambaye kwa sasa anatesa na wimbo wake ‘Too much’ amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anafanya vizuri kutokana na changamoto mbalimbali alizopitia kwenye maisha yake ambazo zimempelekea kufanya kazi kwa kujituma ili asirudi nyuma tena.

darasa732

Darasa anasema moja ya vitu ambavyo vilimpa changamoto ya kupambana ni pamoja na yeye kukosa chakula, sehemu ya kulala hata kukosa malazi ndiyo vitu ambavyo vinazidi kumpa hasira mpaka sasa ya kuendelea kufanya vyema katika kazi yake ya muziki.

“Changamoto zina njia mbili zinaweza kukuua kabisa au zikakufanya kuwa bora zaidi, lakini siku zote mtu mwenye malengo changamoto haziwezi kumuua bali zinamfanya kuwa bora zaidi. Kazi yoyote nzuri ambayo saizi inafanya vizuri ni kutokana na changamoto ambazo nimepitia nyuma, kama kulala njaa nyumbani, ama kukosa sehemu ya kulala au kukosa kitu cha kuvaa na chochote kile ndiyo kimenijenga mimi kuwa mtu bora ambaye ninajua nini cha kusema, nini cha kufanya na wapi kwa kwenda” alisema Darasa.

Mbali na hilo Darasa amewataka vijana kuwa na malengo ya maisha na kutokatishwa tamaa na changamoto ambazo wanakutana nazo bali wanapaswa kupambana nazo ili kufikia malengo yao.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364