Diamond Afungukia Ishu Yake ya Kuripoti Polisi
Msanii Diamond ameelezea kile kilitokea baada ya picha kusambaa zinazomwonyesha akihojiwa na jeshi la polisi.
Muimbaji huyo amedai alienda polisi kujieleza kwa jeshi la usalama barabarani baada ya jeshi hilo kudaka clip yake ya video inayomwonyesha aliendesha gari huku akiwa hajavaa mkanda.
Diamond ametoa taarifa hii kupitia ukurasa wake wa instagram
Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia…?