-->

Diamond, Mobetto Waibua Mabifu ya Mastaa

IMESHAFAHAMIKA kuwa Dylan au Abdulatif ni mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto, siri hiyo iliyofichwa kwa muda mrefu ilifichuliwa na Chibu Dangote mwenyewe katika mahojiano na moja ya redio kubwa nchini.

Baada ya Diamond kuweka bayana ukweli wote mashabiki na watu maarufu mbalimbali nchini wamekuwa na maoni yao huku kila mtu akiwa upande wake ambapo wengi wametokea kumuelewa zaidi Diamond Platnumz.

Kiu kubwa ya Hamisa Mobetto ilikuwa ni kuionyesha jamii kuwa hadanganyi, anasema ukweli kuhusu kubeba ujauzito wa Diamond ndiyo maana ilimlazimu kutumia nguvu ya ziada katika kuonyesha picha na video za chumbani akiwa na Chibu wakati anafahamu wazi hayo hayakuwa makubaliano yao.

Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa alihitaji iwe siri, japo ingekuja kufahamika lakini si kwa mtindo ambao Hamisa aliutumia unaotengeneza mazingira mabaya kwa makuzi ya mtoto wao na mzazi mwenzake na Diamond (Zari).

Sakati hilo limekuwa kubwa na kuzua gumzo kwa mastaa wengine ambao nao wametoa mtazamo wao kuhusu uhusiano huo.

Watu wengi wakiwemo mastaa na viongozi mbalimbali wametokea kumkubali Diamond Platnumz kwa uamuzi wa kukubali kubeba majukumu yote ya baba kama kuhudumia ujauzito mpaka mtoto alipozaliwa.

Miongoni mwao ni mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Mbongo Fleva Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi (Chadema), mwigizaji Shamsa Ford na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Mastaa wengine ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye kwa sasa mwigizaji. Pia kuna waliowahi kuwa wapenzi wa mastaa Barnaba (Zuumela) na Faiza Ally, mzazi mwenzake na mkongwe wa Hip Hop ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi.

ZUUMELA AMTUPIA DONGO BARNABA

Huyu ni miongoni mwa mastaa walioguswa na ujasiri wa Diamond Platnumz wa kukiri kosa na kukubali kuomba radhi kutokana na tukio la kumsaliti na kuzaa nje ya uhusiano wake na Zari.

Mrembo huyo ambaye aliachana na Barnaba miezi kadhaa iliyopita na kuwa na mpenzi mwingine anayemwita (), aliandika hayo kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambayo yalionekana wazi kuwa ni dongo kwa X wake huyo.

Aliandika: “Wanaume wote wangekuwa kama Diamond Platnumz na Kevin Hart walaah hata mimi ningekuwa bado kwenye mahusiano yangu, acha nikapambane na husband wangu mpya.”

Mwisho alimalizia kwa kuwatakia mashabiki mchana mwema huku akisisitiza mpenzi wake mpya hapendi uswahili kwa kuwa kuna watu wanasubiri aseme chochote ili wakazue gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

FAIZA ALLY

Mwanamitindo Faiza Ally yeye aliandika: “Naona umeona aibu mtoto mdogo kama Diamond anavyoweza kuwa ‘responsible’ na watoto pamoja na ujinga wote unaoendelea, haya na aibu ikakushika kuona kuna watoto uliowazidi umri wanakuzidi akili.”

 

Aliandika mengi ambayo yalionekana wazi kuwa na nia ya kumkashfu mzazi mwenzake, Sugu juu ya suala zima la kutomjali mtoto wao wa kike Sasha, madai ambayo amekuwa akiyarudia mara kwa mara.

Hata hivyo, Sugu kupitia ukurasa wake wa Instagram alionyesha kuwa tuhuma hizo si za kweli kwani amekuwa akilipa ada ya shule ya mwanaye huyo licha ya mzazi Faiza kuweka vikwazo ikiwa ni pamoja na kumkataza kuonana na mwanaye.

Sugu alikwenda mbali zaidi kwa kuweka stakabadhi za malipo ya ada jambo lililozima tuhuma hizo za Faiza.

Katika posti hiyo, Sugu aliandika: “Huwa sipendi kuposti mambo haya lakini imenibidi, hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwenye shule ya chekechekea aliyokuwa anasoma mwanangu za mwezi wa 5 mwaka huu 2017 ambako alishamaliza.

“Mwezi huu ilikuwa nimhashie Shule ya Feza pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema hahitaji tena nilipe ada na hata kunizuia nisimuone tena mwanangu Sasha!

“Na ana uwezo wa kumlipia ada ambapo niliwasiliana na uongozi ili niweze kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumwona mwanangu bila sababu… # hivi kama ni nyie mngefanyaje?”

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364