-->

Dogo Janja Amjibu Haya Young Dee (VIDEO)

Baada ya Rappa Young Dee kuomba asifananishwe na wasanii kama Dogo Janja kutoka Arusha na Young Killer wa Mwanza, Dogo Janja amesema hawezi kumjibu msanii huyo kwani hajui kama atakuwa anamjibu mtu mwenye akili timamu au tayari amekula unga.

Kupitia kipindi cha eNewz ya EATV, Dogo Janja amesema kuwa Young Dee kuomba asifananishwe na msanii kama yeye ni sawa kwani hata yeye hataweza kukubali kufananishwa au kukaa na m tu anatumia dawa za kulevya kitu kinachomfanya we anazungumza vitu vya ajabu

“Young Dee ni Mteja, na hawezi kufanana na mimi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee. Akiacha Unga ndo ninaweza kuzungumza kitu kuhusu yeye, kwa sasa hivi nikimzungumzia siwezi jua kama ntakua nabishana nayeye au mteja. Mtu mwenye akili timamu unamsamehe tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine” Dogo Janja.

Dogo janja ameongeza, kuwa hakatai kufananishwa na mtu lakini inatakiwa aangaliwe ni mtu aina gani ambaye anafananishwa naye kwani si kila mtu ni sahihi kufananishwa nae.

“Mimi pia sipendi kufananishwa japo sijakataa kufananishwa, Young Killer mimi nilishawahi kuwa role model wake  kwa hiyo kufananishwa naye si kitu kibaya lakini kunifananisha na mla unga ni kukosea……. Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani kuzungumza lakini kufananishwa naye sasa hivi sitaki kwani ni mtu ambaye ukumuacha gheto unawaza kama utaikuta TV ” amesisitiza.

Hivi karibuni Young Dee alifunguka na kutoa onyo kwa watu na watangazaji kuwa wasimfananishe na Ma Rapaa kama Dogo Janja na Young Killer kwani yeye anafanya mziki mkubwa huku akitoa maneno makali kuwalenga.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364