-->

Dully Sykes Amtetea Harmonize Kumuiga Diamond

Msanii Dully Sykes ametoa maoni yake baada ya tetesi za Harmonize kumuiga Diamond, mara baada ya watu kuzidi kutoa maoni yao baada ya kuachia video yake aliyomshirikisha.

dully

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya EATV, Dully Sykes alianza kwa kutetea kuwa hawafanani lakini baadae akaja kubadilisha upepo,na kusema Harmonize ana kila sababu ya kufanana na Diamond, kwani wasanii hao ni kama ndugu, hivyo sio kitu kibaya wakifanana kwenye baadhi ya mambo.

“Wana tofauti kwa sababu huyu hajazaliwa na koo la Diamond, kitu wanachomfanya wamfananishe na Diamond, hata mimi ukikaa na mtu sana utafanana nae kwa namna moja au nyingine, huyu Diamond ni kaka yake, anaishi na diamond anakaa na diamond, muache afanane nae”, alisikika Dully Sykes akimtetea Harmonize.

Hivi karibuni msanii huyo ameshushiwa tuhuma za kufanana au kuiga kama mashabiki walivyodai, kutoka kwa msanii Diamond Plutnumz, kuanzia anavyoimba mpaka mitindo ya kucheza.

Kwa upande wake Harmonize amekanusha kumuiga Diamond, kwani yeye hawezi kuwa kama Diomond.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364