-->

Duma Kuirudisha Bongo Muvi

Msanii wa filamu bongo, Daudi Michael maarufu kama ‘Duma’ amesema lengo la yeye kumuita nchini msanii kutoka nchi ya Australia John K ni kutaka kuirudisha hadhi ya filamu ambayo imepotea kwa kipindi kirefu katika macho ya watu.

Duma amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV muda mchache baada ya kumpokea mgeni wake huyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

“Watanzania wanapaswa watupe ushirikiano sana katika kazi zetu, nimemleta John K ili niweze kuridisha heshima ya filamu nchini nchini Tanzania na kuonesha jinsi gani Duma anavyopanda kwaajili ya ‘industry’ nasio kwa mtu mmoja mmoja”, amesema Duma.

Pamoja na hayo, Duma ameendelea kwa kusema “sina matatizo na mtu yeyote, lakini naona hii hatua ya kumuita John K tutafika tunapotaka kwasababu John K muda huu Australia na nje ya Australia anafanya vizuri sana”

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364