-->

Dume Suruali Yavunja Historia ya Mwana FA

Video ya wimbo Dume Suruali wa Mwana FA aliyomshirikisha Vanessa Mdee imevunja historia ya rapa huyo kwa kuwa video yake ya kwanza katika historia yake ya muziki kufikisha watazamaji wengi zaidi katika mtandao wake wa ‘You tube’

Video ya ‘Dume suruali’ ilitoka rasmi tarehe 25 Novemba mwaka jana na mpaka sasa imefikisha jumla ya watazamaji zaidi ya milioni mbili, jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye kazi za nyuma za Mwana FA.

Kwa upande wake Mwana FA anasema ni namba flani ndogo kwa wasanii wengine lakini kwake yeye ni kitu kikubwa hivyo hawezi kusema ni jambo la kawaida au kusema hivi ndivyo tunafanyaga bali anawashukuru mashabiki kwani yeye mwenyewe ni kama haamini kile anachokiona.

“Najua, kwamba siyo namba kubwa hii kwa baadhi ya wasanii, actually ni ka-namba flani kaduchu tu, ila kwangu its a big deal kwa hivyo sitakaa niigize hapa kuwa ‘this is how we do it’ na ‘it’s normal’ no it’s not, siyo kawaida..NASHANGAA..AHSANTENI SANA..how about tukifika 3m tunatoa ngoma nyingine? now lets get to 3m..shukrani sana!…Nawaombea wiki njema mahangaikoni… #DumeSuruali” Mwana FA.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364