-->

Ebitoke Afunguka Mapya Kuhusu Mahusianao yake na Ben Pol

Msanii wa vichekesho bongo ambaye inasemekana yupo kwenye mahusiano na msanii Ben Pol, amesema kipindi mahusiano yao yalipoonekana yamekufa, ukweli ni kwamba penzi hilo halikufa isipokuwa Ben Pol alimtuliza ili asiyaweke sana kwenye mitandao.

Akizungumza na mwandishi wa EATV.TV, Ebitoke amesema baada ya kulalamika kuwa Ben Pol hapokei simu zake na hamjali, Ben Pol alimuomba yaishe na aache kuyaweka kwenye mitandao na vyombo vya habari, kwani ni jambo ambalo sio zuri sana kwao.

“Watu walidhani labda tumeachana, hatukuachana na Ben Pol, isipokuwa baada ya mimi kulalamika ile hapokei simu zangu, tulizungumza yaishe na yakaisha, na akaniomba nisiweke sana kwenye mitandao na vyombo vya habari, kwa hiyo tulikuwa sawa ingawa sio kama ambavyo ilikuwa mwanzo”, amesema Ebitoke.

Wawili hao wameanza kuonekana pamoja tena baada ya kimya hiko, huku wakisema wana mipango mikubwa ya kusaidiana kwenye kazi zao za sanaa ambazo ndio zinazowaingizia pesa.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364