-->

Fid Q Afungukia Kupiga Chini Gemu

MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda ‘Fid Q’ hivi karibuni amefunguka kuwa yeye si wa kuacha muziki leo wala kesho maana muziki ni sehemu ya maisha yake na ataufanya mpaka pale Mungu mwenyewe atakapoamua kuwa aachane nao.

Akichonga na Uwazi baada ya kuuliza juu ya kuachana na muziki siku moja na kufanya mambo mengine alizidi kufunguka kuwa, suala hilo ni gumu kwake na hata siku moja hajawahi kuliwazia.

“Unajua muziki ni maisha yangu, sasa sijawahi kabisa kufikiria siku moja niachane na muziki, ninachofikiria ni namna ya kuzidi kuwa bora kwenye muziki na kufika mbali zaidi ya hapa,” alisema Fid Q.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364