-->

Fid Q ataja sababu ya wana hip hop kufeli

Mkali wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ametaja sababu ya wana hip hop kufeli katika kufikisha ujumbe kwa jamii.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Fresh’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa wana hip hop wengi wanafanya muziki kwa ajili ya wenzao na siyo jamii.

“Wana hip hop wanafeli kufikisha muziki mbele kwa sababu wanafanya muziki kwa sababu ya wana hip hop wenzao, hawafanyi kwa ajili ya jamii,” amesema Fid Q.

“Kwa maana hiyo ngoma nyingi unakuta zimejaa majigambo, hayo mambo haumuuzi mtu, ongea na mtu katika lugha yake, mfahamishe Ukimwi ni hatari, mfahamishe kuhusiana na mapenzi, wizi haufai ongea vitu vyake,” ameongeza.

Fid Q bado anazidi kutamba na kugonga vichwa vya habari kupitia Fresh Remix aliyowashirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364