-->

Flora, Ha-Baba Warudiana

DAR ES SALAAM: Mastaa wawili Bongo ambao walikuwa wanandoa kisha wakatengana kwa muda, Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ na Flora Mvungi, hatimaye wamerudiana na sasa ni mwendo wa mahaba niue.

Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ na Flora Mvungi

Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, wawili hao wamerudiana hivi karibuni ambapo hivi sasa ni mahaba niue kwani hata kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakiweka picha wakiwa kimahaba, tofauti na siku zilizopita.

Baada ya kupata ‘unyunyuzi’ huo, Wikienda lilimtafuta H.Baba ambaye alisema kuwa ndoa yake ina amani na hajawahi kutamka kwamba ametengana na Flora.

“Ninachojua ni kwamba ndoa yangu ina amani na iko sawa kabisa, hizo habari za kutengana siwezi kuzizungumzia maana sijawahi kusema tumetengana licha ya Flora kukiri,” alisema H.Baba.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364