Gigy Money Adai Alikiba Alikuwa Anamhonga Vizuri Kuliko Wanaume Wengine
Video queen Gigy Money amedai kati ya wanaume wake wote hawezi kumsahau Alikiba, kwani muimbaji huyo wa Aje ndiye mwanaume wake ambaye alikuwa anamhonda vizuri kuliko wanaume wake wengine.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Gigy amedai aliweza kusoma kutokana na pesa ambazo alikuwa akihongwa na muimbaji huyo.
“Mimi kuwa naye nilikuwa napata kitu sikuwa pale bure bure, na kusema kweli alikuwa ananihonga kuliko wanaume wote na nilikuwa nasoma,” alisema Gigy.
Mrembo huyo amedai anahisi Alikiba hajataka awe video queen kwenye video zake kutokana na kuwa naye kwenye mahusiano katika kipindi cha nyuma.
Bongo5