Gigy Money: Unene Ulikuwa ni wa Utoto
MWANAMUZIKI na muuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameeleza kuwa unene aliokuwa nao awali ulikuwa ni wa utoto hivyo kukonda kwake kwa sasa ni utu uzima.
Akizungumza na Za Motomoto News, Gigy Money alisema watu wanamsema kwa kukondeana kwake lakini anachoweza kusema ni kwamba unene wa zamani ulitokana na mwili wa kitoto lakini hivi sasa amekua mtu mzima.
“Katika familia yetu hakuna mtu mnene hata mmoja, wote ni wembamba hivyo ule mwili niliokuwa nao awali ulikuwa ni wa utoto lakini sasa hivi nimekua ndiyo maana nimepukutika na siyo vinginevyo kama watu wanavyonishambulia kwa maneno mabaya,” alisema Gigy Money.