-->

Hakeem 5 Agoma Kumuomba Alikiba Msamaha

Msanii wa bongo fleva Hakeem 5 amesema hawezi kumuomba Ali Kiba msamaha kwa kuwa hajafanya kosa lolote na alichoongea kuwa Ali Kiba anaroho mbaya aliongea ukweli.

kiba844

Akiongea ndani ya eNewz amesema anaweza kuishi akiwa anafanya muziki na hata  asipofanya hivyo anaweza akaishi hivyo hawezi kwenda kumuomba Kiba msamaha kwa kuwa yeye hakutaka kufanya kolabo na Kiba ila Kiba ndiye alimuomba wafanye kolabo.

Hata hivyo Hakeem 5 hakusita kumjibu Abby Skills na kumuambia kuwa aache unafiki na aendelee na mambo yake kwani hajui chanzo na angekuwa anataka amani angekaa akawapatanisha kama ndugu na siyo kukaa na kuanza kumkandamiza kwenye vyombo vya habari.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364