-->

Harmonize Adaiwa Kumuoneshea Ishara Mbaya Meneja wa Harmorapa Wakiwa Studio

Taarifa iliyotolewa na Kituo cha East Africa Television kupitia ukurasa wao wa Twitter imeeleza kuwa, Msanii kutoka WCB, Harmonize ilikuwa awepo kwenye kipindi cha FNL cha televisheni hiyo usiku huu, lakini ameingia mitini baada ya kumuona meneja wa msanii Harmorapa maeneo ya studio hizo.

Inadaiwa kuwa baada ya kumuona meneja wa Harmorapa, msanii Harmonize amemuoneshea kidole cha kati ambacho hudaiwa kuwa ni ishara ya tusi kisha akaondoka maeneo ya studio hizo.

Aidha Harmorapa amelaani kitendo hicho cha udharirishaji na kudai kuwa Harmonize amemtukana bosi wake kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha kati baada ya kukutana.

Kwa upande wao, kituo cha EATV, kupitia Twitter kimeomba msamaha kwa watazamaji wake wote kutokana na kitendo hicho cha aibu kilichofanywa na msanii huyo.

 

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364