Harmorapa Afungukia Kuvaa Gauni
Msanii Harmorapa ambaye sasa ana ‘trend’ na moja ya video ikimuonyesha akicheza wimbo akiwa amevaa gauni amefunguka na kusema yeye hajavaa gauni la bosi wake kama ambavyo watu wanadai bali yeye amevaa nguo ya kawaida katika video hiyo.
Harmorapa amesema hayo katika kipindi cha eNewz na kudai kuwa yeye alifanya ‘cover’ ya kitu alichofanya Alikiba kwa kuimba wimbo wa ‘Brenda Fassie’ na kwa kuwa yeye anamkubali sana msanii huyo alivutiwa naye na ndiyo maana aliamua kufanya na yeye.
“Unajua mimi namkubali sana Alikiba hivyo nilivyoona amefanya kitu kile na mimi nikasema ngoja nifanye kama ‘Cover’ ila sikuvaa gauni la bosi wangu wala sikuvaa gauni mimi naona niliva mavazi ya kawaida tu, labda nyinyi ndiyo mnaona gauni lakini kwangu mimi ile ni nguo tu ya kawaida” -Harmorapa.