-->

Hata pesa ya kumsaidia Dudu Baya ninayo – Mr. Nice

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mr. Nice amesema anajua kwa sasa Dudu Baya ana hali mbaya ila kama msanii huyo anatajitokeza yeye yupo tayari kumsaidia ili aweze kuendelea na muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye kipindi cha nyuma alikuwa na ugomvi mkubwa na Dudu Baya, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anapoishi nchini Kenya amekuwa akisaidia watu wengi hivyo hataona tabu kufanya hivyo kwa Dudu Baya.

“Napenda kumpa salamu nyingi, napenda kumuombea kwa Mungu abadilike amekua mtu mzima sasa fanye muziki. Ajitokeze afanye muziki na mimi nipo tayari kumsapoti kwa sababu hata pesa ya kumsaidia Dudu Baya ninayo, najua hayuko vizuri, hivyo naweza kumsaidia” amesema Mr. Nice.

Hata hivyo amesema kuwa msaada huo ni hadi pale atakapokidhi vigezo na masharti na kuongeza kuwa kitendo cha Dudu Baya kumfuata jukwaani kipindi cha nyuma na kumpiga kimefanya watu wengi kumuogopa na kushindwa hata kumsaidia pindi anapokuwa na shida.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364