-->

HERI MUZIKI NA DIVA: vipi tena?? “WAAMABIE”

Ikiwa zimepita siku chache toka muimbaji wa Bongo Fleva Heri Muziki kuachia ngoma yake aliyowashirikisha Mwana FA na Mr Paul “Waambie” imeonekana kama mtangazaji Diva thee bawse ambaye ni mpenzi wake kuamua kutoa kipande cha Heri Muziki katika wimbo huo na kuweka sauti yake.

Kutokana na hiki alichokifanya Diva thee Bawse lakini wimbo huo kimetafsirika kama bifu kati yake na Heri Muziki baada ya penzi lao kuripotiwa kuyumba siku chache zilizopita, na wote kukiri hivyo, Diva katika wimbo wa ‘Waambie’ inadaiwa katoa mchango mkubwa, hivyo kukata kipande cha Heri Muziki kunaonesha wazi kuwa ana haki na wimbo huo.

Diva na Heri Muziki wamekuwa wakigombana mara kadhaa katika mapenzi yao lakini hivi karibuni baada ya Diva kuoneshwa kukasirishwa na kitendo cha Heri Muziki kutotaka kukiri radioni kama Diva ni mpenzi wake, kinadaiwa kuyumbisha penzi hilo na inawezekana wasirudiane.

Unaweza kuusikiliza wimbo wenyewe hapa

Comments

comments

Post Tagged with , ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364