Isha Mashauzi Aibukia Kwenye Bongo Flava
Msanii wa muziki miondoko ya taarabu nchini Isha Mashauzi ameamua kuanza kuimba muziki wa dansi pamoja na Bongo Flabva ili kukonga nyoyo za mashabiki wake kutoka kila upande.
Akizungumza na eNews ya EATV Mashauzi amesema ameshafanya video ya wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Jiamini” na umepokelewa vizuri sana na mashabiki kutokana na idadi ya watu ambao wamemtafuta na kumpongeza kwa uamuzi wake huo wa kuleta ladha tofauti na siyo kujikita kwenye taarabu tuu.
“Kwa sasa nimeachia video mpya ya wimbo unaoitwa ‘Jiamini’ wimbo ambao upo katika miondoko ya dansi na tayari nimeona mwitikio wake kutoka kwa mashabiki baada ya kuiachia nimepewa pongezi nyingi na ninawaahidi kwaqmba bado nitatoa ngoma kali na hivi karibuni nitaachia ngoma ya Bongo Flava inayoitwa ‘Nibembeleze” Amesema Mashauzi
“Sitaki nimlazimishe mtu kusikiliza taarabu wakati hataki ndiyo maana nimeamua niimbe pia upande mwingine ili niweze kuwapata mashabiki wa pande zote”- Amesema Isha Mashauzi
Aidha msanii huyo amesema kwa sasa hana mume bali ana mtoto mmoja wa kumzaa na wengine wa ndugu zake jambo ambalo watu wengi hawalifahamu.