-->

Janga Nililonalo ni Ugonjwa – Chid Benzi

Rapa Chid Benzi ambaye siku kadhaa zilizopita amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa amefunguka na kusema janga alilokuwa nalo ni ugonjwa ambao bado anaendelea kupigana nao kuondoa.

Rapa Chid Benzi baada ya kutoka rehab

Chid Benz amesema kuwa katika kipindi cha katikati alifikia hatua ya kuchanganyikiwa na kusema hicho ndiyo kitu ambacho kilimfanya kurudi tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya, ila sasa anasema anapamba kupigana na hali hiyo ili arudi kwenye hali yake kama kawaida na kuanza kufanya muziki.

Unajua kwanza hili janga ambalo mimi niko nalo ni ugonjwa na ni ugonjwa ambao ni mgumu sana, halafu vilevile unaendana na kichwa cha mtu na maisha halisi ya mtu jinsi anavyoishi, kwa hiyo ugonjwa wenyewe unaendana na vitu ambavyo unafanya kila siku mpaka unajikuta unaingia tena kwenye mambo hayo. Kwangu mimi kuna vitu vingi ambavyo vilichanganyikana hapo katikati vilivyopelekea mimi kuchanganyikiwa na kurudi kule, lakini bado ni gonjwa ambalo mimi napambana nalo kuliondoa napigana nalo kwa hiyo watu wajue Chid anapigana nalo hili jambo” alisema Chid Benzi

Mbali na hilo Chid Benz anasema saizi yupo sawa na ameamua kutulia kabisa

“Kama unavyoniona saizi niko freshi na niko sawa kabisa nimeona bora nitulie tu, watu wanatakiwa kunipongeza kwa sababu nimekuwa nikionyesha nia ya kupigana na hili jambo” alisema Chid Benzi

Rapa Chid Benzi alikuwa rehab Iringa na baadaye alikwenda Tanga katika harakati za kupigana na matumizi ya madawa ya kulevya.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364