-->

Joh Makini Akwepa Ishu Hii ya Fid Q

Msanii wa hip hop kutoka Kundi la Weusi, Joh Makini, amesita kuzungumzia issue ya ushindani kati yake na rapa kutoka Mwanza Fareed Kubanda ‘Fid Q’.

Mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiwashindanisha wawili hao, kutokana na uwezo wao wa kuandika mistari na kuchana, hali ambayo imetengeneza taswira ya kwamba huenda hawana maelewano.

Mtangazaji JJ wa Jembe Fm ya Mwanza, alipiga stori na Joh Makini na kumuuliza kama ushindani wake na Fid Q umekwisha baada ya hivi karibuni wawili hao kuonekana hawana tatizo.

“Actually ni vitu ambavyo sipendi kuvipa nafasi, kwa sababu siamini katika hivyo vitu kwenye muziki wangu, toka nimeanza mpaka nimefika hapa,” alijibu Joh Makini.

Rapa Fid Q hivi karibuni alidai kwamba hakuwa na ushindani na rapa huyo wa Kundi la Weusi ambaye kwa sasa, wimbo wake wa ‘Ya kulevya’ unafanya vizuri.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364