-->

Juma Nature Amshushia Lawama TID, Kisa KR Kuokotwa Akiwa Chakari

Msanii wa muziki na kiongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family, Juma Nature amemtupia lawama mkurugenzi mkuu wa Rada Entertainment TID kwa tuhuma za kumuaribu KR Muller.

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

KR ambaye zamani alikuwa katika Kundi la TMK Wanaume Family na Juma Nature, aliondoka katika kundi hilo mapema mwaka huu na kujiunga na Rader Entertaiment iliyo chini ya mwanamuziki TID.

Juma Nature amedai alfajiri ya Jumapili alimkuta KR akiwa hajitambui kwa kuzidiwa na kilevi nje ya baa maarufu maeneo ya Mwembeyanga, Temeke.

“Alfajiri nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwamba ndugu yako tumemkuta huku kalewa, hajitambui kwa kuwa yeye alishaondoka kwenye kundi sisi tulibaki wenyewe kwenye kundi na kina Dolo, tukaona si vibaya tukodi taxi impeleke kwake anakoishi sasa,” alisema Juma Nature aliliambia gazeti la Mwananchi.

Nature amesema alipopigiwa simu alfajiri ya Jumapili, ilimrudisha kukumbuka ya nyuma namna alivyomshauri kukaa mbali na matendo yasiyofaa na makundi mabaya.

“Binafsi sijachukulia vizuri yeye ni kioo cha jamii na nilishamshauri huko anakohamia, kwa sababu tangu yupo kwetu alikuwa na matatizo, lakini yamezidi tangu aende huko kwa sababu hivi vitu vinasababishwa na makundi, sasa ukiwa unakaa na makundi ambayo watu wanavyoishi ni tofauti na jamii tayari ni tatizo,” amesema Nature.

Baada ya mkasa huyo, Bongo5 ilimtafuta KR Mulla na kuzungumza naye kuhusiana na mkasa huyo.

“Bwana mimi ni mtu mzima, TID ananiaribu kivipi, ile siku maji yalizidi tu kibinadamu. Lakini nipo safi kabisa wala sina tatizo, kwani ile hali imetokea mara ngapi, vile ni vitu vya kawaida,” alisema Mulla

BONGO5

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364