Jux ameachana na Vanessa Mdee?
Msanii Jux ambaye awali alikuwa akitoka kimapenzi na msanii Vanessa Mdee amefunguka na kusema kwa sasa yeye hayupo single kama ambavyo watu wanakuwa wakisema lakini pia amekanusha zile tetesi kuwa ameachana na mpenzi wake Vanessa Mdee.
Jux alisema hayo jana kupitia kipindi cha Frida Night Live na kusema taarifa ambazo zinasambazwa kuwa sasa yupo single si kweli japo alishindwa kunyoosha maelezo kama ni kweli ameachana na Vanessa au bado wapo pamoja.
“Naanza kabisa hiyo habari si ya kweli sasa kama habari si ya ukweli unadhani hapo ukweli ni upi? Si kila kitu unachokiona au kukisikia ni cha ukweli, sihitaji kuzungumzia suala hilo la Vanessa kwa sasa, lakini hiyo habari si ya kweli saizi mimi vitu vingi nimebadilika, hivyo nina kila uhuru wa kusema kwa hiyo kwanza nakusahihisha ile stori siyo ya kweli mimi siyo ‘single boy’ kwa hiyo kama ikiendelea hiyo habari iendelee lakini mimi nathibitisha kuwa hiyo habari si ya kweli” alisema Jux
Mbali na hilo Jux alipatwa na kigugumizi kujibu swali moja kuhusiana na Vanessa Mdee, baada ya mtangazaji kumuuliza kama anaendelea kutoka na Vanessa, Jux alipojibu swali hilo alisema hayo ni mambo yake binafsi.
eatv.tv