-->

Kinachomsumbua Roma Mkatoliki

Rapa Roma Mkatoliki aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na tungo zake zenye kugusa jamii na maisha ya kila siku ya watu, amefunguka na kusema toka ametekwa na kuachiwa afya yake kiujumla imeimarika ila bado anatatizo katika kidole chake cha mwisho.

Roma Mkatoliki anadai kuwa kidole hicho kilivunjika lakini hata baada ya kufanyiwa matibabu bado kidole hakijaweza kukaa sawa kwani kimekuwa hakina mawasiliano lakini hakiwezi kumzuia yeye kuendelea na michakato mingine akiamini kuwa ipo siku atapata wataalam ambao wataweza kukinyoosha kidole hicho.

“Unajua niliumia sehemu nyingi ila sehemu ambayo bado haijakaa sawa ni kwenye kidole kwani nilivunjika kwenye kidole cha mwisho tunachokiimba kilivunjika ndiyo maana utaona nilikuwa na muongo muda mrefu zaidi ya wiki sita, tumefungua hongo lakini kama hakijaunga bado hivyo ni kama hakina mawasiliano hakikunji wala hakifanyi chochote, lakini hiki hakinizuia mimi kufanya mambo mengine, Inshalaah kila kinachotokea Mungu huwa na sababu zake labda Mungu hapendi ninyooshe kidole cha mwisho juu tena jukwaani japo siamini katika hilo panapo majaliwa tutapata wataalam wakinyooshe kitakaa sawa” alisema Roma Mkatoliki

Mbali na hapo Roma Mkatoliki anasema mtandao wake wa Instagram ulikuwa ‘hacked’ siku mbili baada ya wao kuachiwa huru na mateka hivyo saizi anahangaika kuhakikisha wanairudisha account yake hiyo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364