Kufanya Collabo na Man Fongo ni Hadi 2020- TID
Msanii wa Bongo Fleva nchini TID amesema atakuwa tayari kufanya kazi na msanii maarufu wa Singeli nchini Man Fongo ifikapo mwaka 2010 na siyo kwa sasa.
TID ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa, na kuweka bayana kwamba kwa sasa ana mambo mengi na kzi nyingi za kufanya hivyo hataweza kufanya Colabo na msanii huyo.
“Nitakuwa tayari mwaka 2020 na siyo sasa pamoja na kwamba utakuwa mwaka wa uchaguzi lakini ndiyo kitakuwa kipindi kizuri cha kufanya hivyo lakini kwa sasa hivi sipo tayari nina kazi nyingi nazifanya” Amesema TID
TID ameklazimika kuyasema hayo kufuatia ujumbe mfupi wa mtazamaji wa EATV aliyetaka kujua kama TID atakuwa tayari kufanya Colabo na Man Fongo.