-->

Kuna watu wamekuja kuuharibu muziki wetu – Matonya

Msanii mkongwe wa muziki, Matonya amewataka wadau mbalimbali wa muziki kuwa makini na watu ambao wamekuja kuuharibu muziki wa bongofleva.

matonya02

Muimbaji huyo ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Vaileti’ na nyingine nyingi, ameiambia Bongo5 kuwa kuna vijana wameingia kwenye muziki bila kuwa navipaji.

“Mimi napenda kuwapongeza wasanii wote wazuri ambao wanafanya vizuri lakini kuna watu pia hawastahili kupongezwa kwa sababu wamekuja kuuharibu muziki wetu,” alisema Matonya. “Kwahiyo wanaokuja kwa matusi kwa nia ya kuuharibu muziki tutawachukia sana,”

Aliongeza,“Kuna watu wamekuja kuuharibu muziki wa bongofleva. Kwa sababu tunaona kabisa kuna watu ambao walikuwa hawana ajira wamepata ajira. Sisi ambao tumefanya muziki huu kwa muda mrefu tumeona mafanikio pamoja na connection. Lakini kuna watu ambao hawajiwezi wanakuja na wanafanikiwa kwenye muziki, kwahiyo tukiwaruhusu kuuharibu muziki wetu kwa njia yoyote watakuwa wameharibu chakula cha watu wengi,”

Pia muimbaji huyo wiki hii ameachia wimbo mpya ‘Mr Legeza Kidogo’ wa wasanii wa kundi lake jipya liitwao ‘Black Image’.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364