-->

Latifa Ilimtuliza Mwenye Kichaa – Mb Dog

Msanii Mb Dog amesema kwamba wimbo wake wa Latifa ulimpa historia kubwa kwenye maisha yake, ikiwemo kumtuliza mwanamke ambaye alikuwa na kichaa cha mimba.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mb Dog amesema wakati ametoa wimbo huo na kufanikiwa kufanya vizuri, alienda Mwanza kwenye show na kukutana na mzee mmoja ambaye alimfuata akimuomba akasalimie familia yake, kwani amekuwa mtu muhimu kwao.

Mb Dog aliendelea kusema kuwa alipoenda kuwasalimia ndipo akaonyeshwa mama akiwa na mtoto mchanga, na kupewa kisa ambacho mzee huyo alilazimika kumpa mtoto huyo jina la Latifa ili kumpa heshima Mb Dog.

Msikilize hapa chini akisimulia mwanzo mwisho

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364