-->

Madam Flora Atoa Ujumbe Huu Kwa Wote

Ikiwa leo ni mwezi mmoja na siku kadhaa toka msanii wa Injili Madam Flora kufunga ndoa kwa mara ya pili na mume wake Daudi Kusekwa baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha, Fora amefunguka na kuwataka watu kuwa na maamuzi binafsi.

Madam Flora akiwa na mumewe Dauki Kusekwa

Msanii huyo amewataka watu kuwa na maamuzi binafsi kama wanataka kufikia ndoto zao na kudai kuwa unaweza ukawa unamshirikisha mtu lakini mtu huyo asiwe na nia njema na wewe hivyo anaweza kukushauri ndivyo sivyo.

“Jifunze kuwa na maamuzi yako binafsi, sio kila jambo lazima ushirikishe watu ndipo ulifanyie maamwuzi kwani si kila unayemshirikisha anakuwazia mema. Pokea ushauri vizuri kabisa lakini jifunze kuwa na maamuzi binafsi ili kutimiza ndoto yako” alisema Madam Flora

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364