-->

Mapya Kutoka kwa Lady Jaydee

Mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa tayari ana album nzima iko ndani na anachofanya ni kutoa kazi moja moja kila baada ya miezi mitatu.

Lady JayDee

Lady Jaydee

Leo kupitia kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio. Lady Jaydee amesema album yake imekamilika na inaitwa ‘Woman’ hivyo hata huu wimbo mpya ni kutoka katika album hiyo.

Lady Jaydee amesema wazo la wimbo huo sawa na wao alilipata kutokana na maisha ya watu wake wa karibu ambao amekuwa akiishi nao katika maisha ya kila siku.

“Unajua mimi nina marafiki mbalimbali wa rika zote, wapo walionizidi sana umri, wapo nalingana nao na wengine ni wadogo zangu kabisa hivyo muda mwingi napotoka nao au kujichanganya nao ndipo nikapata wazo la wimbo huu ‘Sawa na wao’ kwani binadamu tunatofautiana. Saizi nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa kazi moja kutoka kwenye album yangu hiyo ya ‘Woman’. Alisema Lady Jaydee

Katika hatua nyingine Jaydee amesema kwamba wimbo wa Sawa na Wao’ ambao anazungumzia maisha halisi katika jamii huku ukiwa na lugha ya kiswahili na kikongo katika mahadhi ya lingula ameurekodi disemba mwaka jana na imani yake ni kwamba hata waangusha mashabiki katika kazi ambazo anazitoa na atakazozitoa.

”Idea imetokana na maisha ninayoishi, kila mtu ana tabia zake mimi nina tabia zangu na mwingine ana tabia zake lakini tukikutana tunakuwa wamoja” Amesema Lady Jaydee.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364