-->

Martin Kadinda Atoa Siri ya Wema

Mbunifu maarufu wa mavazi bongo ambaye pia ni mtu wa karibu wa Wema Sepetu, Martin Kadinda, ametoa siri kwa wasiomjua mlimbwende huyo maarufu kama Tanzania Sweetheart ni mkorofi kuliko anavyoaminika.

Wema Sepetu na Martin Kadinda

Kadinda ametoa siri hiyo ambayo wengi walikuwa hawajui kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba Wema Sepetu yuko tofauti na watu wengi wanavyoamini kuwa yupo, lakini pia udhaifu wake mkubwa ni kumuamini kila mtu bila kuchukua muda kumjua zaidi.

“Wema ni mkorofi kutoka ndani, lakini anajitahidi kadri ya nguvu zake ukorofi wake usionekane, na akiamua kukorofisha anakorofisha kweli, kuna matukio mimi nikisikia amefanya najua huyu walimgusa sehemu mbaya, kingine ambacho Wema anacho ana ‘open door’, milango ya moyo wake iko wazi, yuko wazi sana ni rahisi kumuamini mtu, atakujua leo na kesho ukawa rafiki yake na ukalala kwake”, amesema Martin Kadinda.

Hivi karibuni mrembo huyo ambaye alifanikiwa kuchukua taji la Miss Tanzania mwaka 2006, ameamua kuacha kuweka mambo yake wazi na kujikita kwenye kazi zake za sanaa, ambapo sasa ana movie mpya sokoni inayoitwa ‘Heaven sent’.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364