-->

Martin Kadinda: Diamond Hakukosea Mavazi Kwenye video ya ‘Salome’

Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda amefunguka kwa kusema kuwa Diamond hakukosea kuvaa mavazi aliyovaa kwenye video yake ya wimbo ‘Salome’ baada ya watu katika mitandao ya kijamii kudai mavazi hayo hayakuendana na uhalisia ya video hiyo.

diamond832

Mbunifu huyo ambaye pia amekuwa akimvalisha msanii huyo, amesema hakuona tatizo kwa Diamond kutumia mavazi yale kwa kuwa ni mavazi ambayo yamekuwa yakitumika zaidi Afrika.

“Mimi nimependa kwa sababu hajavaa nguo kutoka China lakini amevaa nguo za kiafrika kwa sababu sisi sote ni waafrika,” alisema Martin. “Lakini hayo malumbano niliyasikia katika mitandao ya kijamii na sikutaka kuyaingilia kwa sababu mimi naamini kile alichokifanya tayari alikuwa team ambayo ilikuwa inamshauri,”

Pia mbunifu huyo amewapongeza wasanii kuamua kuwatumia wabunifu mbalimbali katika kazi zao huku akiitaka serikali kuipa nguvu tasnia hiyo ya ubunifu.

Martin ni mmoja kati ya wabunifu ambao watashiriki kuonyesha mavazi yao katika tamasha kubwa la mavazi nchini, Swahili Fashio Week.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364