-->

Matonya: Sibahatishi Kwenye Muziki

Msanii wa Bongo Fleva Matonya amesema kuwa yeye kwenye muziki habahatishi anajua nini anafanya na kwamba sasa amepunguza kufanya show za nje ili kijipa nafasi ya kuandaa kazi zake mpya pamoja na video mbalimbali ambazo zitaanza kutoka muda si mrefu.

Matonya

Matonya amesema haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio ambayo ilikuwa ikiruka moja kwa moja kutoka Tegeta Nyuki Dar es Salaam ambapo Matonya amedai kuwa mpaka sasa ameshafanya kazi kibao kali ambazo bado ziko ndani.

“Kwa sasa nimesimama kusafiri sana na kufanya show nje ili kujipa nafasi ya kurekodi kazi nyingi na kutengeneza video za kutosha, mimi kwenye muziki sibahatishi hivyo mashabiki zangu msiwe na wasiwasi nimeshafanya kazi nyingi na kubwa zipo ndani nasubiri muda tu nianze kuachia moja baada ya nyingine na kwa kuanzia leo hii nawakabidhi video pamoja na audio ya ngoma yangu mpya ambao ni safi na salama, na kuanzia sasa itakuwa ni bandika bandua sitaki kuwaacha mashabiki na kiu ya kazi tena” alisema Matonya

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364