-->

Meneja Maneno Naye Atafuta Meneja wa Kumsimamia

Msimamizi wa siku nyingi wa wasanii wa Muziki Tanzania Meneja Maneno amesema anatafuta mtu wa kufanya naye kazi kama meneja wake kwa sasa.

maneno

Meneja Maneno

Amesema anatafuta meneja kwa kuwa mbali na kwamba bado yuko kwenye kitengo cha umeneja katika ofisi yake na bado anasimamia baadhi ya wasanii kama vile Nay wa Mitego, kwa sasa na yeye ameamua kuwa msanii.

Akiongea ndani ya eNewz Maneno amesema kwa sasa ana kazi nyingi hivyo anahitaji mtu wa kumsapoti katika majukumu yake kwa kuwa anaamini kwamba kidole kimoja hakivunji chawa na ili ufanye kazi nzuri ni lazima apate wasaidizi wazuri.

Maneno amemaliza kwa kusema  ana mpango wa kuachia wimbo wake mpya ambao utaitwa kata funua hivyo anahitaji meneja wa kumsapoti kwa kuwa “ukiamua kuwa msanii ni lazima upate mtu wa kukusimamia kazi yako ili ufanye vizuri” Amemalizia kwa kusema ana kazi  nyingi hivyo anahitaji sapoti.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364