-->

Mh. Temba: Sijawahi Kubebwa na Chege

Msanii wa bongo fleva Temba amesema maneno yanayoongelewa kwamba anabebwa kimuziki na msanii mwenzake Chege hali inayompelekea ashindwe kuachia nyimbo kwa muda mrefu hayana ukweli wowote.

Temba

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Temba amesema kuna biashara alikuwa anafanya na mtu iliyokuwa inahusiana na muziki ambayo mwisho wake aliyekuwa anafanya naye biashara alimizimia simu na kumkimbia hali iliyopelekea kushindwa kutoa nyimbo kwa wakati.

Pia Temba aliendelea kusema kwamba hawezi kuwazuia watu kuongea kwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kuongea lakini ukweli ni kwamba wimbo wake ulikuwa utoke hata kabla ya wimbo wa Chege ‘Waache waoane’ na ‘Kelele za chura’.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364