Mke Wangu Ameolewa Kabla Sijampa Talaka – Nuh Mziwanda
Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda amedai Baby Mama wake, Nawal alishinikizwa kuolewa na wazazi wake kabla hata ajampatia talaka.
Muimbaji huyo amedai ingawa tayari aliyekuwa mke wake huyo ameshaolewa mtu mwingine lakini bado hajampatia talaka ya kusema kwamba wameachana.
“Mimi sijaachana na Nawal, mpaka sasa mimi sijatoa talaka kusema mimi wewe sikutaki endelea na maisha yako.,” Nuh aliimbia Times Fm. “Lakini kulikuwa na msuguano wa hapa na pale ambao naamini haukuwa unatokana na mimi na yeye, ulitokana na familia yake. Kwahiyo haikuwa kwamba mimi simtaki Nawal yeye hanitaki mimi ila familia yake ndio iliyosimamia huu mchongo,”
Nuh alisema ingawa hajamuacha Nawal lakini sio mke wake tena kwa sababu tayari ameshaolewa na mwanaume mwingine.
Wawili hao walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye, ‘Anyaghile’
Bongo5