-->

Mpoto Afungukia Kutembea Peku Peku

Msanii wa muziki wa kughani nchini Tanzania, Mrisho Mpoto amefunguka kwa kudai hapendi kuwa ‘mpumbavu’ na ndiyo maana anatembea peku peku (bila ya kuvaa viatu) popote pale aendapo na hakuna mtu wa kumzuia kutofanya hivyo.

 

Mpoto amebainisha hayo baada ya kuwepo na tetesi kuwa alizuiwa kuingia kwenye nje za ughaibuni wakati anakaguliwa kwenye lango la kutokea uwanja wa ndege katika siku hivi karibuni.

“Kwa kuna mahusiano gani kati ya mimi kuvaa viatu na kutoa vaa eenh ?, mimi ‘i feel comfortable’ kama nikikanyaga ardhi na kutengeneza ‘connection’ kati ya ardhi na mwili wangu pamoja na akili yangu. Kwa sababu mahusiano ya ardhi yanajenga akili kwa hiyo mimi nahitaji kuwa na akili sitaki kuwa mpumbavu” amesema Mpoto.

Pamoja na hayo, Mpoto amesema yeye hawezi kufanana na wasanii wengine wanaotoa wimbo mpya kila baada ya miezi miwili kwa kuwa yeye anatumia muda mwingi katika kufikili kuandika tungo zake.

“Kazi hii siyo rahisi jamani, ni ngumu kufikili tunajitahidi sana na mimi najitahidi kupambana kama mnavyoona tokea nitoe Sizonje huu mwaka wa pili sasa. Mimi na watu wengine ni tofauti hatufanani, hatuweza kufanana kwa sababu kuna wao halafu kuna mimi”, amesema Mpoto.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364