-->

Mr. Nice Amchana Dudu Baya, Adai Hana Mhahali pa kuishi

Msanii Mr Nice ambaye kwa sasa ameachia kazi yake mpya ya Yaya, amejibu tuhuma za msanii mwenzake Dubu Baya aliposema kwamba maisha yamemshinda na kukimbilia Kenya, na kumjibu kuwa Dudu Baya ni msanii asiyejielewa, ndio maana hana mahali pa kuishi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teleivison, Mr.Nice amesema ni wakati sasa Dudu Baya akomae na game kama anavyofanya yeye, kwani muda wa malumbano na kuchafuana hautamsaidia chochote, na hastahili kufanya hayo kwakuwa umri umeshamucha.

Mr. Nice ameendelea kwa kusema kwamba Dudu Baya ni mlevi na anaishi maisha ya kuigiza, hivyo kabla hajaanza kumuongelea vibaya ni vyema akaanza kujilinganisha naye kama wanafanana kimaisha.
Msikilize hapa chini kisha tazama jiwe jipya la Mr. Nice ‘Yaya’.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364