-->

Mr. T Touchez Amleta Rasmi Harmorapa (VIDEO)

Zikiwa zimepita wiki mbili sasa tangu rapa anayechipukia Harmorapa kukutana na producer anayefanya vyema kwa sasa kwenye sekta ya muziki Mr. T Touchez na kufanya kazi pamoja inasemekana kazi ya rapa huyo iko tayari kwenda mtaani hivi sasa.

Producer T Touchez amefunguka na kusema kazi hiyo imekamilika kila kitu na sasa ipo tayari kwenda kwa wananchi ili waweze kumsikia rapa huyo ambaye baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa hawezi muziki, huku wengine wakimpa moyo kuwa akaze atatoka kwenye muziki na kufanikiwa kama watu wengine.

 

“Harmorapa final mix niambie hii nyimbo niitoe lini? “. Alihoji Mr T Touchez

Awali Mr. T Touchez alipokutana na Harmorapa alimpa ushauri kuwa aache maneno bali anatakiwa kuleta muziki mzuri ili kuweza kukata ngebe za baadhi ya watu ambao huenda hawaamini katika uwezo wake.

Harmorapa mpaka sasa ni kati ya wasanii wachache ambao wanachipukia na kuweza kuwa na kismati cha kupendwa na watu wa lika zote kutokana na namna anavyoishi na jinsi ambavyo yeye mwenyewe anajiweka.

Hadi sasa amefanikiwa kukutana na watu wengi maarufu akiwemo Producer nguli wa muziki wa bongo fleva P Funk Majani, Juma Nature, na Erick Shingongo ambao wote walionyesha kufurahi kukutana na kijana huyo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364