-->

Msami Afunguka Kumtamani Wema Sepetu

Msanii wa bongo fleva ambaye pia ni miongoni mwa ma’dansa’ wakali Bongo, Msami Baby ameweka wazi hisia za moyo wake na kusema kuna mastaa wa ‘bongo movie’ anatamani kutoka nao kimapenzi.

Msanii huyo amesema katika tasnia ya filamu ametokea kuwapenda wadada watatu ambao ni Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) na Jokate Mwegelo japokuwa amekuwa matatani kwa kushindwa kuchagua mmoja kwa kuwa wote ni wazuri.

“Katika mastaa wa bongo ambao ninawapenda sana na ninatamani ningewapata ni pamoja na Jokate Kidoti, Lulu na Wema Sepetu, uzuri wa hawa wadada unanifanya niwapende sana” Alisema Msami

Kwa upande mwingine msanii huyo amesema yeye umri kwake siyo kigezo kikubwa kwakuwa ameshawahi kutoka na mwanamke aliyemzidi umri na wakaishi vizuri bila ya kuwa migogoro ya aina yeyote ile.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364