Naachia Ngoma ya Hip hop Mwaka Huu – Bob Junior
Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka Sharobaro Records Bob Junior ametangaza rasmi kuwa mwaka huu anataka kuachia ngoma ya Hip hop kwa sababu yeye ni Rapa na anauwezo huo.
Bob Junior alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kudai kuwa mwaka huu ataachia kazi mbili, moja ikiwa ni ya kuimba na nyingine ataonesha uwezo wake wa kuchana.
“Unajua mimi ni Rapa hivyo mwaka huu nitaachia kazi yangu mpya ya kuimba ambayo itakuwa na ‘Sound’ mpya kabisa kutoka Sharobaro Records lakini pia nitaachia kazi yangu nyingine ambayo nimechana mwanzo mwisho” alisema Bob Junior
Mkali huyo kutoka Sharobaro ameshindwa kutoa video ya kazi yake aliomshirikisha msanii Jose Chameleone na kudai kuwa ratiba za Chameleone zimekuwa nyingi na kufanya mipango ya video ya kazi hiyo kuwa migumu hivyo plan B ameamua kutengeneza video ya kazi yake nyingine ambayo imeshakamilika na itatoka muda wowote.
eatv.tv