Najivunia Kufananishwa na Jay Z- Joh Makini
Msanii wa miondoko ya ‘Hip hop’ kutoka kampuni ya Weusi, Joh Makini amefunguka ya moyoni na kusema anajisikia faraja kwa mashabiki zake kumfananisha na msanii Jay Z.
Joh Makini amesema ufananisho huo uko wazi kwa kuwa kiwango cha muziki wake ni mkubwa kiasi ambacho watu wanaomzunguka na wapenzi wa kazi zake hawaoni mtu mwingine wa kumfananishia naye isipokuwa msanii huyo kutoka Ughaibuni.
“Jay Z ni ‘role model’ wangu…mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika ‘level’ ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye…Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z ‘yeah i like it’ kuliko ungenifananisha na mtu mwingine”. Alisema Joh Makini
Kwa upande mwingine msanii huyo amedai changamoto na vikwazo anavyokutana navyo katika kufanya kazi zake za kila siku huwa ndiyo vinamfanya aweze kutengeneza mambo mazuri zaidi.