-->

Nawaonea Huruma Kizazi cha Sasa – Fid Q

Msanii mkubwa wa hip hop bongo Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, amesema anasikitishwa na hatama ya maisha ya kizazi cha sasa, kwani kimeharibiwa kwa kiasi kikubwa na mitandao.

Fid Q

Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20 cha kinachorshwa na East Africa Radio, Fid Q amesema kizazi cha sasa hakina muda kabisa wa kujisomea vitabu ili waweze kujiongezea ujuzi, kwani mabadiliko ya teknolojia yamechukua sehemu kubwa ya maisha yao.

“Nawaonea huruma sana watoto wa kizazi hichi, mtu anatoka mapumziko anakutana na stori ya Alikiba katoa fresh remix, itamvuruga kabisa kwenda kuzingatia somo la hesabu ambalo linafuatia, sijui tunafanyaje lakini nawaonea huruma sana, sababu mi ni zao la analojia”, alisema Fid Q.

Fid Q ambaye kwa sasa yupo na kazi mbili sokoni ambazo ni ‘ulimi mbili’ na ‘fresh’, amesema kwa kipindi hiki cha digitali anapata changamoto kubwa anaposoma vitabu mitandaoni, kwani muda mwengine hukutana na matukio mengine yanayomfanya asitishe zoezi hilo, tofauti na kama angekuwa anasoma kitabu cha kawaida.

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364